Majaliwa:Rais Dkt.Magufuli ametoa mwelekeo mpya wa kiuchumi, kiutawala

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametoa mwelekeo mpya wa kiuchumi na kiutawala nchini ambao umesababisha Tanzania iingie kwenye kundi la nchi za uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliopangwa wa 2025, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono, kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ziendelee kutoa elimu ya uchumi wa viwanda kwa wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu kujenga na kukuza uchumi wa viwanda.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 14, 2021) katika ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma alipozindua kitabu cha “The Game Changer: President Magufuli’s First Term in Office”. Kitabu hicho kimehaririwa na Profesa Ted Maliyamkono na Dkt. Hugh Mason.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono (kulia) kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono (kulia) baada ya kukizindua kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. Kushoto ni Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Amesema mpangilio na muktadha mzima wa kitabu hicho unabeba dhamira ya kukifanya kuwa kimbilio la rejea kwa watunga sera, wafanya maamuzi, wanataaluma na hata wananchi wa kawaida katika masuala mazima ya maendeleo ya nchi yetu. 

“Kitabu hiki tunachokizindua leo, The Game Changer, kimeonesha namna sera na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano ilivyobadili mwelekeo wa Taifa letu kimaendeleo. Nitoe rai kwa waandishi wa kitabu hiki, waangalie uwezekano wa kutoa chapisho kwa Kiswahili ili Watanzania wengi waweze kukisoma na kunufaika na maudhui yake.”
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono, kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu amesema kitabu kimefafanua kuwa Tanzania ni nchi yenye kuendeshwa kidemokrasia na kimeondoa shaka waliyonayo wadau wa maendeleo na wawekezaji kwa lengo la kuwawezesha kuongeza uwekezaji wao hapa nchini. 

Naye, Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Balozi Mhandisi Dkt. John Kijazi amesema: “Kitabu hicho kiwe chachu kwa Maprofesa wa vyuo vingine, wakae chini wafanye tafiti na kuandika vitabu vya aina hiyo ili kusaidia kuhifadhi historia ya nchi.” 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Katibu Mkuu, Kiongozi, Mhandisi, John Kijazi nakala ya kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono baada ya kukizindua kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Amesema vitabu vya aina hiyo vitasaidia vijana kutambua kazi zilizofanywa na viongozi mbalimbai nchini pamoja na kuenzi historia ya nchi. 

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kazi ya fasihi andishi ni kutunza kumbukumbu na kitabu hicho kitasaidia kuhakikisha mambo mazuri yaliyofanywa na Rais Dkt. Magufuli yanadumu kwa vizazi vijavyo. “Hakika kazi yake imetukuka.” 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Viongozi mbalimbali baada ya kuzindua kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono, kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Naye, Mhariri Mkuu wa kitabu hicho, Profesa Maliyamkono akisoma muhtasari wa kitabu hicho, amesema kimeelezea namna Rais Dkt. Magufuli alivyoingia madarakani, hali aliyoikuta na hatua alizochukua pamoja na mafanikio ya Serikali. 

“Rais Dkt. Magufuli wakati anaingia madarakani aliikuta nchi ikiwa katika wakati mgumu kiuchumi, amefanya kazi kubwa ya kurekebisha mikataba mibovu ya madini, amedhibiti rushwa na kwa sasa nchi inafaidika na rasilimali zake. Hakuna kiongozi wa Afrika ambaye aliweza kuziwajibisha kampuni kubwa za madini lakini Rais Dkt. Magufuli ameweza.” 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Viongozi mbalimbali baada ya kuzindua kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Awali, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitoa maoni kuhusu utendaji kazi wa Rais Dkt. Magufuli alisema amefanya mambo mengi katika miaka 20 ya utumishi wake Serikalini na miaka mitano ya urais. “Rais Dkt. Magufuli ni muasisi wa wazo la ujenzi wa barabara kwa kutumia fedha za ndani.” 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipunga mikono kuaga baada ya kuzindua kitabu cha " The Game Changer: President Magufuli's First Term in Office" kilichohaririwa na Profesa Tedi Maliyamkono, kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma, Januari 14, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema Rais Dkt. Magufuli ni mwanamageuzi wa kweli na ameipambanua nchi katika miradi mikubwa kama ya ujenzi wa reli ya kisasa inayowawezesha Watanzania kushindana katika uchumi. Alishauri kuwe na maandiko mengi yahusuyo viongozi. 

Kitabu kimetayarishwa kwa lengo la kuweka kumbukumbu ya kazi zilizofanyika na zile zilizotegemewa kufanyika katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano (2015 - 2020) chini ya Rais Dkt. Magufuli. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news