Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today January 23rd, 2021

 Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku wa leo tarehe 23-01-2021 unaletwa na mchambuzi Happiness Mpunza kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).Weather forecast

Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight on today January 23rd, 2021 as presented by analyst Happiness Mpunza from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 23/01/2021

Mikoa ya Kigoma, Katavi, Songwe, Mbeya, Rukwa na Njombe: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.........

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu,Tabora, Singida, Ruvuma na Iringa: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.........

Mikoa ya Dar es salaam, Pwani(ikijumuisha visiwa vya Mafia), Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

........

Mikoa Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba, Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Dodoma: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.......


VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

MJI               Kiwango cha juu     Kiwango cha chini 

                     cha  joto                 cha joto

ARUSHA       28°C                       16°C

D'SALAAM   32°C                        25°C

DODOMA     29°C                       20°C

KIGOMA       29°C                       21°C

MBEYA         27°C                      16°C

IRINGA         28°C                      17°C

NJOMBE      20°C                       13°C

MWANZA    29°C                       19°C

TABORA       29°C                       18°C

TANGA         31°C                       22°C

ZANZIBAR    32°C                       25°C

..........

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa  kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini, na kwa kasi ya km 20 kwa saa kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi madogo hadi Makubwa kiasi.

Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 25/01/2021: mabadiliko kidogo

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 23/01/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

MATARAJIO YA HALI MBAYA YA HEWA KWA SIKU TANO ZIJAZO.
JUMAMOSI: 23/01/2021
ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa.
UWEZEKANO WA KUTOKEA: WASTANI
KIWANGO CHA ATHARI ZINAZOWEZA KUTOKEA: WASTANI
.........
Athari zinazoweza kujitokeza:
Pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za uvuvi.
.........
Tafadhali zingatia na ujiandae.
........
JUMAPILI: 24/01/2021 HADI JUMATANO :27/01/2021
HAKUNA ANGALIZO

Imetolewa leo 23/01/2021

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news