This is Simba SC...Mtibwa Sugar yachapwa mabao 5-0

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameichapa Mtibwa Sugar 5-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Mabao ya Simba SC katika mtanange huo wa Aprili 15,2021 yamefungwa na nyota wa kigeni Clatous Chama dakika ya tisa, Rally Bwalya dakika ya 19, Mnyarwanda Meddie Kagere dakika ya 43 na 52 na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 69.

Kutokana na ushindi huo Simba SC inayofundishwa na Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa inafikisha alama 49 baada ya kucheza mechi 21 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa alama mbili na Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi ya Wekundu hao.

Post a Comment

0 Comments