Norway yaahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kukuza uchumi,kuwaletea wananchi maendeleo

NA BENNY MWAIPAJA,Washington DC

SERIKALI ya Norway imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika hatua zake za kukuza uchumi na kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia miradi mbalimbali ambayo nchi hiyo inafadhili katika sekta za nishati, kusaidia kaya maskini na usimamizi wa fedha za umma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wa ili kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango - Zanzibar, Mhe. Saada Mkuya Salum (kushoto) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango – Zanzibar. Dkt. Juma Malik Akil, wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Norway anayesimamia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa, Bi. Anne Tvinnereim, walipokutana kando ya mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Washington DC, Marekani.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Norway anayesimamia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa, Bi. Anne Tvinnereim, kando ya mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Washington DC, Marekani.

Alisema kuwa tangu mwaka 2010, Norway imewekeza nchini Tanzania zaidi ya shilingi bilioni 300 kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo iliyosaidia kuboresha maisha ya watu na kuchangia agenda ya mabadiliko iliyowekwa na Serikali katika kuinua Maisha ya watu wake.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alisalimiana na Waziri wa Norway anayesimamia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa, Bi. Anne Tvinnereim, walipokutana kando ya mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Washington DC, Marekani.

“Serikali ya Norway imeahidi kwamba itaendelea kushirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya nishati hususan usambazaji wa umeme vijijini, mabadiliko ya tabia nchi na kusaidia sekta ya fedha za umma,” alisema Dkt. Nchemba.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bi. Anne Tvinnereim, alisema kuwa nchi yake imeridhishwa na utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na nchi yake ikiwemo kuzisaidia kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Waziri wa Norway anayesimamia masuala ya Maendeleo ya Kimataifa, Bi. Anne Beathe Tvinnereim (katikati), akimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), walipokutana kando ya mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Washington DC, Marekani.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Washington DC).

Aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kusaidia mpango huo wa TASAF pamoja na kuangalia maeneo ya kuboresha hifadhi ya mazingira ambayo ni changamoto kubwa inayochangia mabadiliko ya tabia nchi.

Dkt. Nchemba anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF inayofanyika jijini Washington DC nchini Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news