Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Aprili 20, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 17.8 na kuuzwa kwa shilingi 17.9 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 153.8 na kuuzwa kwa shilingi 155.3.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Aprili 20, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.

Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.3 na kuuzwa kwa shilingi 2310.15 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2972.8 na kuuzwa kwa shilingi 3003.4.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2468.2 na kuuzwa kwa shilingi 2493.8 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 358.05 na kuuzwa kwa shilingi 361.2.

Kwa mujibu wa BoT, shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.8 na kuuzwa kwa shilingi 19.9 huku Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.

Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.8 na kuuzwa kwa shilingi 628.9 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) inanunuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.
Kwa upande wa Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1682.9 na kuuzwa kwa shilingi 1700.5 huku Pula ya Botswana (BWP) inanunuliwa kwa shilingi 195.8 na kuuzwa kwa shilingi 197.1.

Kwa mujibu wa Benki Kuu, dola ya Canada (CAD) inanunuliwa kwa shilingi 1810.3 na kuuzwa kwa shilingi 1827.8 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.06 na kuuzwa kwa shilingi 50.51.

Post a Comment

0 Comments