Waziri Aweso awasimamisha kazi watumishi wanne Wizara ya Maji

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Aweso amefanya kikao na wadau wa Sekta ya Maji wa Handeni na kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ikiwemo kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne wa Wizara ya Maji kutokana na kusuasua kwa kazi ya ujenzi wa Bwawa la Kwankambala.
Kikao hicho kilichofanyika Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi wa Wilaya ya Handeni ni moja ya hatua zilizochukuliwa baada ya ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Aweso wilayani humo Aprili 12, 2022 ambapo ilibainika kwamba Mhandisi anayejenga bwawa hilo amelipwa Shilingi milioni 602.8 sawa na asilimia 3 ya gharama ya mkataba na kazi iliyofanyika ni asilimia 20 tu.

Pia iligundulika kwamba kampuni iliyopewa kandarasi ya kazi hiyo iitwayo Civil Loth Enterprises Ltd iliondoa vifaa vya kazi katika eneo la ujenzi, ingawa ilikuwa imeongezewa muda wa utekelezaji wa ujenzi na kutokana na hali hiyo, kikao kilichoongozwa na Aweso kimeelekeza kufanyika kwa mapitio ya Mkataba wa nyongeza wa Mkandarasi.

Aidha,hatua nyingine ni kuwasimamisha kazi watumishi wafuatao ili kupisha uchunguzi, Hamisi Matungulu (Msimamizi wa Mradi – RUWASA Makao Makuu), Jimmy Mwanyakunga (Mhasibu Mkuu – RUWASA Makao Makuu),

Amos Mtweve (Meneja Udhibiti Ubora wa Miradi na Mwenyekiti wa Bodi ya Manunuzi RUWASA Makao Makuu), Zam Mlimira (Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi – RUWASA Makao Makuu).

Kwa mujibu wa taaarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Wizara ya Maji, Bw.Florence Temba hatua nyingine ni kama;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news