WAZIRI DKT.MABULA AADHIMISHA MIAKA 60 YA KUZALIWA, ACHANGISHA MILIONI 41.6/- ZA MASOMO KWA WANAFUNZI WENYE UHITAJI

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ameadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwake kwa kuchangisha fedha shilingi milioni 41,616,500 za kugharamia masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Dkt.Angeline Mabula (wa pili kushoto) akiwa ameshika bilauri ya mvinyo wakati wa kuadhimisha miaka 60 ya kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022. Kushoto ni Askofu wa Jimbo la Mtwara, Titus Mdoe na kulia ni aliyekuwa katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi.
Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara, Titus Mdoe akizungumza wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt.Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Aidha, ameitaka jamii kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wenye uwezo wa kimasomo lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kifedha.

Maadhimisho hayo yamefanyika Mei 6, 2022 mkoani Dodoma kwa Waziri Dkt Mabula kushiriki Misa Takatifu kwenye Kanisa la Parokia ya Uwanja wa Ndege na kufuatiwa na chakula cha hisani kilichofanyika Hoteli ya ST Gasper.

‘’Tukiwa na utaratibu wa kuasaidia basi tutakuwa tumewasaidia wanafunzi wengi wenye uwezo wa kimasomo, lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto za kifedha,’’ amesema Dkt.Mabula.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt.Angeline Mabula (Kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama (kushoto) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi wakiwa kwenye Misa Takatifu Parokia ya Uwanja wa Ndege Dodoma wakati wa kuadhimisha kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa Dkt.Mabula. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022. Kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe.

Alisema, lengo la kuitumia siku yake ya kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa kwake kuchangisha fedha ni kutaka kuwanufaisha wanafunzi kwenye taaluma mbalimbali na kutaka kila mtu kutoa michango kulingana na alivyoguswa.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe alimsifu Dkt Mabula kwa uamuzi wake wa kutoa shukurani kwa Mungu kwa zawadi ya uhai aliyoipata kufikisha miaka 60 sambamba na uamuzi wa kuchangisha fedha za kusaidia masomo jambo alilolieleza kuwa ni uamuzi wa busara.

‘’Mama ana jambo lake naye ni mpenzi wa masikini wa roho na mali ndiyo maana umechagua kuwasaidia masikini, vijana wanaokosa pesa za ada lakini umeamua kushiriki kutafuta pesa za kuwasaidia’’ alisema Askofu Mdoe.
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa Mhe. William Lukuvi akizungumza wakati kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Mhe.Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Allan Kijazi (Kulia) wakifurahia jambo wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Askofu Mdoe alibainisha kuwa, wapo vijana wengi waliopo vijijini lakini wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na hali ya wazazi wao jambo lililomsukuma Waziri Dkt Mabula kuja na wazo la kuchangisha fedha wakati wa misa ya kusheherekea kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa.

Baadhi ya wanafunzi walionufaika na mfuko huo wa kichungaji walieleza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa fursa za kimasomo kwa wale wanafunzi wanaotoka familia za kimasikini.

Thomas Kichenje anayesoma Stashada ya Utawala wa Biashara Chuo cha STeMMUCo Mtwara alisema, bila ya ufadhili wa mfuko wa kichungaji asingekuwa chuoni hapo kwani baada ya kuomba vyuo kadhaa alikosa ufadhili.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete akitetea jambo na Waziri wake Dkt Angeline Mabula wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Dkt Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa tatu kushoto) akiongoza zoezi la kula keki wakati wa kuadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wakinyanyua bilauri yenye mvinyo wakati wa kuadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Mwanafunzi mwingine Frank Kiwanga anayesomea masomo ya sheria chuo cha SAUT Mtwara alieleza kuwa, alikosa mkopo wa elimu ya juu mara nne lakini kupitia msaada wa mfuko wa kichungaji ameweza kusoma shahada hiyo.

Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa Dkt Mabula kwa kuchangisha fedha yamefanyika pia katika mikoa ya Mbeya, Mwanza na Mtwara. 

Uchangiaji wa mfuko huo unafanyika kwa wananchi kununua kadi za kuchangia, udhamini wa wanafunzi, mchango wa hisani kupitia chakula ambapo fedha zinazochangwa hutumika kulipia gharama za Bweni, Ada , Bima pamoja na Mafunzo ya Vitendo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. Safi sana Waziri Mabula Mungu akubariki sana

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news