Rais Samia atoa maelekezo kwa Makatibu Mahsusi, Watunza Kumbukumbu na Maafisa Utumishi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Makatibu Mahsusi, Watunza Kumbukumbu pamoja na maafisa Utumishi kutunza siri za Serikali.

Ametoa wito huo leo wakati akifungua Mkutano wa Tisa wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
Makatibu Mahsusi kutoka Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakiimba na kushangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 02 Juni, 2022.

Aidha, Rais Samia amesema suala la utunzaji wa siri za Serikali linasaidia kuepuka madhara yanayoweza kuwapata watu binafsi, Taasisi, Serikali na usalama wa Taifa letu.

Rais Samia pia amesema weledi, uaminifu, uadilifu na uzalendo ndiyo njia pekee itakayowafanya Makatibu Mahsusi kuaminiwa, kutegemewa na kuwawezesha kusonga mbele katika majukumu yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Zawadi Maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) Bi. Zuhura Songambele Maganga kabla ya kufungua Mkutano huo Mkuu wa Kitaaluma kwa Makatibu hao Mahsusi kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 2 Juni, 2022.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameridhia Chuo cha Utumishi wa Umma Tabora kuwa maalum kwa ajili ya mafunzo ya uhazili kwa ngazi zote ili kuzalisha Makatibu Mahsusi ambao watakwenda kutumika katika Taasisi za Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Makatibu Mahsusi wa Ofisi mbalimbali za Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Kitaaluma uliondaliwa na Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) kwa ajili ya Makatibu hao nchini katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Conventional Centre Jijini Dodoma tarehe 2 Juni, 2022. 

Halikadhalika, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha miundo mbalimbali ya kada za kiutumishi, na maslahi ya watumishi wa umma kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news