Serikali yazidi kuwaheshimisha wastaafu,warithi na walezi nchini

NA GODFREY NNKO

SERIKALI imesema kuwa hadi Aprili 2022 imelipa mafao na pensheni kwa wastani wa wastaafu 59,825 kila mwezi, mirathi kwa warithi 1,038 yakiwemo malipo ya malezi kwa walezi 1,246 na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishi wa Serikali walio kwenye mikataba 500.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameyasema hayo leo Juni 7, 2022 wakati akiwasilisha bungeni jijini Dodoma, Makadirio ya Mapato na Matumizi ambapo ameliomba Bunge kuiidhinishia wizara yake bajeti ya shilingi trilioni 14.94.

Kati ya fedha hizo shilingi trilioni 13.62 ni matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.32 ni matumizi ya maendeleo kwa mafungu yake nane kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2022/2023

"Wizara imeendelea kuboresha mfumo wa huduma ya pensheni, mirathi, utunzaji wa kumbukumbu, uhakiki wa wastaafu na ulipaji wa mafao na pensheni kwa watumishi wa Serikali ambao siyo wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Pamoja na mirathi na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishi wa Serikali walio katika mikataba na viongozi wa kisiasa,"amesema Mheshimiwa Waziri Dkt.Nchemba.

Aidha, amesema wizara inaendelea kufanya uhakiki wa wastaafu wote wanaopata malipo ya pensheni kupitia ofisi ya Hazina.

Post a Comment

0 Comments