Simba SC yakung'utwa na Tanzania Prisons

NA DIRAMAKINI

TANZANIA Prisons wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Nahodha wake, Benjamin Asukile dakika ya 54 na kwa ushindi huo, wanafikisha alama 29 za mechi 29 na kusogea nafasi ya 14. 

Kwa upande wao, Simba wanabaki na alama 60 nafasi ya pili nyuma ya mabingwa tayari, Yanga wenye alama 71 baada ya wote kucheza mechi 29.

Post a Comment

0 Comments