CEO wa Simba SC asema msimu huu wanakomba makombe yote

NA DIRAMAKINI

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa, msimu huu klabu hiyo imejipanga kurudisha makombe yote ya ndani na kuhakikisha inafika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
CEO wa Simba Barbara Gonzalez Kushoto akizindua Slogan mpya kwa msimu huu ya 'We Are Unstoppable' (Kushoto) ni malkia wa Bongo Fleva Zuchu.

Barbara ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa Simba Week uliofanyika Mbagala Zakheim jiini Dar es salaam ambapo pia ameongeza kuwa usajili bado unaendelea na kuanzia wiki ijayo wataendelea kushusha wachezaji wengine.

“Safari hii hakuna kuteleza tena. Tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mataji yote kuanzia Ligi Kuu, FA na kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika,”amesema.

Kuelekea kilele cha Simba Day ambayo itafanyika Agosti 8, 2022 Simba imezindua Slogan Mpya We Are Unstoppable (Hatushikiki Hatuzuiliki).

Msimu uliopita Simba ilizisiwa ujanja na watani zao Yanga baada ya kuzoa makombe yote ikiwemo la Ligi Kuu ya NBC,Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup) na Ngao ya Jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news