Kamisaa wa Sensa afikisha elimu Old Shinyanga

NA MARCO MADUHU

KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi, Mhe. Anne Makinda, ametembelea katika Mnada wa Old Shinyanga, kutoa elimu na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 mwaka huu. 
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.

Makinda ametembelea katika mnada huo Julai 3,2022 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).Akizungumza na wananchi kwenye mnada huo, amewasihi siku hiyo ya zoezi la kuhesabiwa Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 mwaka huu, washiriki kikamilifu ili Serikali ipate idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo kuanzia ngazi ya chini. 

"Tunaendesha zoezi la Sensa ya watu na makazi ili tujue Tanzania tuko watu wangapi, na itaisaidia Serikali katika upangaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wote kulingana na idadi yao,"amesema Makinda. 
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akizungumza katika Mnada wa Old Shinyanga na kutoa elimu ya Sensa kwa wananchi na kuwahamasisha washiriki kikamilifu kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa Agost 23 mwaka huu. 

"Rais Samia Suluhu Hassani amekuwa akitafuta fedha za maendeleo kwa wananachi wake, na anataka kujua ni maeneo gani ambayo wananchi bado hawana maendeleo kwa uwiano sawa na idadi yao, hivyo nawasihi jitokezeni kuhesabiwa Sensa," ameongeza. 

Aidha, amewataka pia wananchi watoe ushirikiano kwa Makarani wakati wa Sensa pamoja na kutoa taarifa za kweli na usahihi na siyo kudanganya ili siku huduma zikianza kutolewa na Serikali katika eneo husika kusiwepo na mapungufu. 
"Kama wewe una ng'ombe 100 wataje wote usiseme una ng'ombe 10, ili siku madawa yakija kulingana na idadi ya mifugo mlioitaja msianze kugombania na kulalamika madawa hayatoshi na wakati awali nyie ndiyo mlitoa taarifa siyo sahihi,"amesema Makinda.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Pastory Ulimali akizungumza kwenye Mnada huo wa Old Shinyanga.Katika hatua nyingine, amewataka wananchi wasiwafiche ndani watu wenye ulemavu pamoja na wazee, bali wawape fursa nao ya kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa. 

Nao baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye mnada huo pamoja na wafanyabiashara, wameshukuru kupatiwa elimu hiyo kuhusu Sensa ya Watu na Makazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news