Mheshimiwa Jenista Mhagama atoa fungu kufanikisha ujenzi zahanati, ofisi

NA MWANDISHI WETU 

MBUNGE wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ameunga mkono jitihada za wananchi wa Kijiji cha Matimira B kilichopo jimboni kwake kwa kuchangia shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na shilingi milioni 1 ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya kijiji hicho.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akichimba msingi kuashiria uzinduzi wa Zahanati katika Kijiji cha Matimira B wakati wa ziara yake iliyolenga kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo. 
Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Matimira wakati wa ziara yake iliyolenga kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Mhe. Jenista ametoa mchango huo katika Kijiji cha Matimira B, wakati wa ziara yake ya kuhimiza ushiriki wa wananchi katika maendeleo na uboreshaji wa huduma za kijamii katika jimbo lake. 

Mhe. Jenista amesema kuwa, akiwa ndiye Mbunge anayewawakilisha wananchi wa Jimbo la Peramiho katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameamua kuwa nao bega kwa bega katika masuala yote yanayohusu maendeleo. 
Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiweka jiwe la msingi la ukarabati wa mradi wa tanki la maji katika Kijiji cha Matimira B wakati wa ziara yake iliyolenga kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Mhe. Jenista ametumia fursa hiyo kumtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi. Neema Maghembe kuunga mkono kwa vitendo jitihada za wananchi pindi wanapoanzisha miradi ya maendeleo ya kijamii kama huo wa ujenzi wa zahanati. 
Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akishiriki kufyatua tofali za mradi wa kikundi cha vijana wa Kijiji cha Mpangula Kata ya Matimira wakati wa ziara yake iliyolenga kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

“Wananchi hawa wamefyatua tofali wenyewe na kuziweka katika eneo la ujenzi, leo tunashiriki nao kuchimba msingi wa ujenzi wa zahanati, hivyo Mkurugenzi na watendaji wako hamna budi kuwaunga mkono ili kukamilisha zahanati hii kwa wakati na kuanza kutoa huduma,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kuzindua nyumba za watumishi wa Kituo cha Afya Matimira wakati wa ziara yake iliyolenga kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Aidha, Mhe. Jenista amesema kuwa, iwapo watajitokeza wadau wa maendeleo ambao wana nia ya kuunga mkono jitihada za wananchi wake yupo tayari kushirikiana nao ili kutimiza lengo la wananchi wa Matimira B la kukamilisha ujenzi wa zahanati itakayotoa huduma kwa akina mama, wazee, watoto, vijana na wananchi kwa ujumla. 
Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na mjasiriamali katika soko la wamachinga, Kijiji cha Matimira baada ya kuzindua soko hilo wakati wa ziara yake iliyolenga kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake, mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Matimira B, Bi. Sylivia Mhagama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mhe. Jenista Mhagama Mbunge kwa kutoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Zahanati hiyo ambayo itawapunguzia mzigo wa gharama ya kusafiri hadi Peramiho au Songea mjini kufuata huduma za afya. 

Naye Bw. Filbert Nkale amesema Kijiji chao kimekuwa kikikabiliana na changamoto ya kukosa zahanati kwa kipindi kirefu, changamoto iliyosababisha akina mama kutopata huduma ya afya ya mama na mtoto hivyo kuhatarisha maisha yao. 
Wananchi wa Kijiji cha Matimira wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake iliyolenga kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Bi. Coltilda Komba, amemshukuru Mhe. Jenista kwa kuzindua ujenzi wa Zahanati ya Matimira B kwani itawawezesha kupata huduma ya afya ya mama na mtoto ambayo imekuwa ikiwakabili kwa muda mrefu. 

Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama ameanza ziara jimboni kwake yenye lengo la kuhimiza ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news