Rais Samia afanya uteuzi Mamlaka ya DSFA


NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Mkurugenz─▒ Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority - DSFA).
Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Dkt. Sweke anachukua nafasi ya Bw. Zahor Kassim El-Kharousy ambaye amemaliza kipindi chake.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Sweke alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).

Taarifa imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza leo Julai 20, 2022. 

Post a Comment

0 Comments