Rais Samia afanya uteuzi SBT,TARI,TTB,AGITIF,CPB,TPHPA,TCDC,TCB na STAMICO

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi za Mazao na Taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Kilimo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kama ifuatavyo:
Mosi, amemteua Bwana Filbert Michael Mponzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT). Bwana Mponzi ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Dar es Salaam.

Pili, amemteua Dkt. Tausi Mbaga Kida kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Dkt. Kida ni Afisa Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Tatu,amemteua Bwana Victor Kilasile Mwambalaswa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB). Bwana Mwambalaswa ni Mbunge Mstaafu na ni Meneja Mradi wa Kampuni binafsi ya Geowind Power Tanzania Limited, Dar es Salaam.

Tano,amemteua Bwana Omar Jumanne Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pembejeo wa Taifa (AGITIF). Bwana Bakari ni Mkurugenzi na Mwanzilishi Mwenza wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tanzania Data Lab (dLab), Dar es Salaam.

Sita,amemteua Bwana Salum Awadh Hagan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB). Bwana Hagan ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya SSC Capital, Dar es Salaam.

Saba,amemteua Prof. Andrew E. Temu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA). Prof. Temu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Trustees of the Private Agricultural Sector Support (PASS).

Nane,amemteua Bwana Abdulmajid Nsekela kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Bwana Nsekela ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.

Tisa,amemteua Bwana Christopher Mwita Gachuma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB). Bwana Gachuma ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Nyanza Bottling Co. Ltd ya Jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 25, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus, uteuzi wa wenyeviti unaanza tarehe 24 Agosti, 2022.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Dkt. Venance B. Mwase kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Kabla ya uteuzi huu Dkt. Mwase alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 25, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus,uteuzi huo unaanzia tarehe 23 Agosti, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news