Mzungu wa Simba SC yamkuta mazito,uongozi watoa tamko nzito usiku huu

NA DIRAMAKINI

BAADA ya aliyekuwa Mshambuliaji wa Simba Mserbia, Dejan Georgijevic kuthibitisha kuvunja mkataba na miamba hao wa soka ikiwa ni muda mfupi tangu alipojiunga nao,uongozi wa klabu hiyo umetoa tamko rasmi.
Nyota huyo aliyesajiliwa na Kocha Zoran Maki ambaye naye aliondoka na kutimkia Misri alijiunga na Simba Agosti 7, mwaka huu akitokea NK Domzale ambapo tangu ametua nchini amekuwa gumzo kubwa kutokana na kuwavutia mashabiki.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Dejan aliandika; "Nathibitisha mkataba wangu na waajiri wangu umevunjika, asanteni sana mashabiki kwa sapoti na mapenzi mliyonipa,"

Nyota huyo anaondoka kwenye kikosi hicho akiwa amefunga bao moja tu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar Agosti 20, wakati Simba iliposhinda mabao 2-0, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Tamko la Simba SC;

Post a Comment

0 Comments