Parachichi, Cocoa, minofu ya samaki kutoka Tanzania ina soko kubwa Ubelgiji-Balozi Nyamanga

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mheshimiwa Jestas A.Nyamanga leo Septemba 21, 2022 amezungumza na waandishi mbalimbali wa habari nchini.
Mheshimiwa Balozi Nyamanga akiwa jijini Brussels nchini Ubelgiji amezungumza na waandishi wa habari kupitia Mtandao wa Zoom,ikiwa ni sehemu ya mikutano mfululizo ya inayoratibiwa na Watch Tanzania kuwakutanisha wanadiplomasia hao na wanahabari kuelezea kuhusu fursa mbalimbali ambazo Watanzania wakishiriki kikamilifu zitaleta matokeo bora kwa jamii na Taifa kwa ujumla.


"Ubeligiji mpaka sasa ina nchi 14 tu duniani ambazo inashirikiana nazo kwenye masuala mbalimbali hasa katika ubia wa maendeleo na Tanzania ni miongoni mwa hizo nchi 14, ambazo ni nchi 13 kutoka Afrika na Mashariki ya Kati moja"

"Katika kipindi cha nyuma 2004 mpaka hivi karibuni nchi ya Ubeligiji imekuwa ikitoa wastani karibu Euro milioni 11 kila mwaka kupitia moja kwa moja serikalini au NGO's zao, miradi iliyonufaika inapatikana Kigoma miradi ya kilimo na mradi wa maji.

"Ubeligiji ni miongoni mwa nchi chache Ulaya ambako Tanzania tunauza bidhaa zetu kuliko Tanzania inavyonunua bidhaa kutoka Ubeligiji na imekuwa hivyo takribani miaka minne mfululizo sasa.

"Tanzania tunauza sana minofu ya samaki nchini Ubeligiji, kwa sasa kupitia minofu ya samaki kutoka Mwanza inaingiza tani 50 mpaka 60 kila wiki ambako inaenda Ubeligiji na kusambazwa nchi zingine.

"Pia kumekuwa na uhitaji mkubwa wa zao la Cocoa kutoka Mbeya huko Kyela na Morogoro ambako inauzwa, hitaji letu kubwa ni kuona nchi nyingi za Ulaya zinanunua Cocoa toka kwetu Tanzania.

"Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuuza parachichi nchi za ulaya ikitanguliwa na South Africa na Kenya, lakini sehemu kubwa ya parachichi zetu tunauza kupitia Kenya, tupo kwenye mazungumzo na taasisi ya TAHA kuangalia namna parachichi ziunzwe moja kwa moja bila kupitia Kenya.

"Ubeligiji ilikuwa na miradi 32 ya uwekezaji mwanzo yenye thamani ya shillingi milioni 902 lakini sasa hivi ina miradi 45 nchini Tanzania yenye thamani ya shillingi milioni 978 ambayo ipo katika maeneo mbalimbali moja ya Kampuni waliyowekeza ni TBL.

"Tumeongea na wawekezaji kutoka Ubeligiji wanaomiliki kampuni ya TBL kujenga kiwanda kingine Dodoma cha kimea chenye thamani ya dola zaidi ya milioni 150 ambacho kikikamilika kitatoa ajira nyingi sana.

"Nchi ya Luxembourg ndio nchi ya Ulaya inayoongoza kwa utoaji wa mikopo ya bei nafuu, hivyo tunawasihi makapuni mbalimbali yanayotaka mikopo kufanya utaratibu na kuwasiliana na ubalozi kupata mawasiliano ya benki mbalimbali za Luxembourg.

"Kuna Shirika linaitwa BIO ambalo linapokea pesa toka Serikali ya Ubeligiji na wako tayari kusaidia mikopo nafuu sana kwa ajili ya wajasiriamali kwenye sekta za uzalishaji, miradi ya nisharti, kilimo na kadhalika, mwaka jana walitupa Euro milioni 3.8 ( shillingi bilioni 8) ambazo zilitumika Tanzania kutoa mikopo nafuu.

"Tanzania ni miongoni mwa nchi 24 duniani ambazo zimepata fursa ya elimu ya Masters na PHD kama scholarship hapa nchini Ubeligiji,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news