Wizara ya Ardhi yatoa ratiba utatuzi wa migogoro ya ardhi jijini Dodoma

NA DIRAMAKINI

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kuwa,inaendelea na zoezi la kampeni ya utatuzi wa migogoro ya ardhi katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuitafutia ufumbuzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt.Allan Kijazi imefafanua kuwa, zoezi hilo lilianzia katika Mkoa wa Dar es Salaam na sasa litaendelea mkoani Dodoma.

"Hivyo, kuanzia tarehe 26 hadi 30 Septemba, 2022, Kamati ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo inashirikisha taasisi mbalimbali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama itaendelea na zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi katika Jiji la Dodoma.

"Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kusikiliza malalamiko ya wananchi, kupokea vielelezo,kufanya uchambuzi wa kitaalam na kuchukua hatua zinazostahili. Inasisitizwa hapa kwamba migogoro itakayofanyiwa kazi ni ile tu ambayo haijawasilishwa mahakamani. Katika kufanikisha utatuzi wa migogoro hiyo, Kamati ya Wataalam imeandaa ratiba ya utekekezaji wa zoezi zi hilo kama ifuatavyo;

RATIBA YA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA JIJI LA DODOMA

Post a Comment

0 Comments