Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wawili.
Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Zaituni Mohammed Haji kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi Serikalini katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

Kabla ya uteuzi huo, Zaituni alikuwa Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi Serikalini. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 20, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Pili, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Mhandisi Ali Said Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Ali alikuwa Msimamizi Mkuu wa Miradi ya Ujenzi katika Wizara ya Afya.Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa viongozi hao unaanza leo Septemba 20, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news