Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo amefanya uteuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 28, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinhi amemteua Mgeni Jailani Jecha kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) katika Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora.

Kabla ya uteuzi huo ambao umeanza leo Septemba 28, 2022 ndugu Mgeni alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Mipango na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Post a Comment

0 Comments