Rais Dkt.Mwinyi aipongeza Serikali ya Cuba

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mheshimiwa Yordenis Despaigne aliyefika Ikulu Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar mgeni wake, Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Yordenis Despaigne, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo.

Rais Dkt. Mwinyi aliishukuru Cuba kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati yake na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kupitia sekta za elimu na afya.

Amesema Taifa hilo limekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Zanzibar kutokana na msukumo mkubwa inayotoa kupitia sekta za Afya na Elimu, ambapo pamoja na kutoa msaada wa madaktari pia hutoa fursa za masomo kwa wanafunzi wa Zanzibar.
Dkt.Mwinyi alimueleza Balozi huyo kuwa, Zanzibar inahitaji kuongeza uwezo wake katika utoaji wa huduma za afya kwa kuwa na madaktari na Manesi baada ya Serikali kujenga hospitali 10 kutoka katika kila wilaya na hivyo akabainisha umuhimu wa kupata fursa za mafunzo.

Aidha, Dkt. Mwinyi alisema Zanziabr itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Cuba katika masuala mbali mbali ya kimataifa.

Naye Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Yordenis Despaigne alisema Cuba inajivunia uhusiano na ushirikiano wa kihistora kati yake na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, na kuahidi kuuendeleza, ili kusaidia juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma na kuimarisha uchumi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mgeni wake Balozi wa Cuba nchini Tanzania,Mhe. Yordenis Despaigne alipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leoSeptemba 1, 2022. (Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news