Waziri Mhandisi Masauni afanya uteuzi Baraza la Taifa la Usalama Barabarani

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemteua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe 18 wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Waziri Masauni amemteua Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Jumanne Sagini kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Wakati huo huo, Waziri Masauni amemteua Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Aidha Waziri Masauni amewateua Wajumbe wa Baraza hilo ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha.

Wajumbe wengine ni pamoja na:-

1. Dkt. Henry Swai

2. Ponziano Lukosi

3. Rogatus Matavila

4. Mhandisi Victor Seff

5. Rtd DCP Mohamed Mpinga

6. Neema Swai

7. SACP Johansen Kahatano

8. Dkt. Baghayo Saqware

9. Mhandisi Yona Africa

10. Isabela Nchimbi

11. Agustas Fungo

12. Faraji Abri

13. Issa Nkya

14. Dorice Mutalemwa

15. Abdallah Miraji

16. Mhandisi Dkt. Phil Makini

17. Anord Mtewele

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 4, 2022 uteuzi huo umeanza Septemba Mosi, 2022.

Post a Comment

0 Comments