EWURA yatoa maelekezo kwa watendaji wa mamlaka za maji nchini

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), Mhandisi Modestus Lumato amewataka watendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira nchini kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na EWURA ili kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Mhandisi Lumato ametoa maelekezo hayo leo Oktoba 10,2022 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa watendaji hao yaliyolenga kuwajengea uwezo katika maandalizi ya mikakati ya utendaji ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.
“Kama mlivyoelekezwa awali, kuja na mikakati yenu inayozingatia miongozo iliyotolewa na EWURA, mafunzo haya yatawawezesha kuboresha mikakati hiyo itakayoongeza ufanisi wa utendaji wenu,”amesisitiza Mhandisi Lumato.

Naye Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira EWURA, Mhandisi Exaudi Fatael, ameeleza kuwa, EWURA imeandaa miongozo husika kwa lengo la kuimarisha huduma hususani katika kudhibiti majanga.

Sambamba na kudhibiti upotevu wa maji pamoja na namna bora ya kuchagua, kufunga, kupima na kutunza dira za maji ikiwemo muongozo wa kushindanisha utendaji wa mamlaka za maji.

Mafunzo hayo yamewakutanisha watendaji kutoka mamlaka za maji 31ikijumuisha mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Tabora,Singida,Iringa, Kilimanjaro, Tanga, Manyara na Morogoro.
Aidha, mafunzo hayo yanafanyika kwa siku nne kwa maana ya leo Oktoba 10 hadi Oktoba 13, 2022 katika ofisi za Makao Makuu ya EWURA jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news