Waziri Dkt.Kijaji:Tunahakikisha viwanda vya nguo vinafanya kazi kwa ufanisi

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji ( Mb) amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha viwanda vya nguo nchini vinavyoajiri watu wengi hususani wanawake na vijana vinafanya kazi kwa ufanisi.
Lengo la Serikali likiwa ni kuongeza ajira, pato la taifa, kukuza biashara ya ndani na nje ya nchi na uchumi kwa ujumla.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha nguo cha A TO Z, Bw. Kalpesh Shah akiwa na Meneja Mauzo ya Nje wa Kiwanda hicho, Bw. Sylvester Kazi leo Oktoba 10, 2022 katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili na kUtatua changamoto zinazoikabili sekta ya nguo nchini.
Aidha, katika kuendeleza sekta hiyo, Dkt.Kijaji amesema Serikaki inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi ili kuhakikisha pamba inayozalishwa nchini inakuwa na ubora unaotakiwa na inatosheleza mahitaji ya viwanda vya nguo nchini kwa mwaka mzima ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Dkt. Kijaji pia amesema ni muhimu kuanzisha viwanda vya kuchakata pamba (spinning) nchini ili kuongeza thamani katika zao la pamba na kupunguza uuzaji wa pamba ghafi ambayo asilimia 70 ya pamba inayozalishwa nchini huwa inauzwa nje ya nchi kama malighafi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news