Rais Dkt.Mwinyi amwakilisha Rais Samia nchini Uganda

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Oktoba 8, 2022 ameondoka kuelekea nchini Uganda katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa nchi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimia na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakati akielekea nchini Uganda kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru wa Uganda, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu).

Rais Dk Mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika ujumbe alioambatana nao ni pamoja na mkewe Mama Mariam Mwinyi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na viongozi mbalimbali wa Serikali Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akielekea nchini Uganda leo kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru wa Uganda, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Uganda zitakazofanyika kesho Jumapili tarehe 9, Oktoba, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news