Waziri Mkuu ashuhudia maendeleo makubwa ya ujenzi wa Meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo Oktoba 17, 2022 ametembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu.
Mpaka sasa mkandarasi ameshalipwa shilingi bilioni 78 na ujenzi wake umefikia asilimia 73. Akizungumza wakati akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Meneja wa mradi huo, Vitus Mapunda amesema tarehe 30 Novemba, 2022 meli hiyo itashushwa majini ili kumalizia kazi ya mifumo ikiwa inaelea.
Aidha Amesema kuwa ifikapo Mei 30, 2023 meli hiyo itakuwa imekamilika na kukabidhiwa.

Post a Comment

0 Comments