Yanga SC uso kwa uso na Club Africain

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Tanzania itakutana na Club Africain ya Tunisia katika mechi ya mchujo wa kuwania kucheza Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika droo iliyopangwa Oktoba 18, 2022 makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Yanga itaanzia nyumbani Novemba 2,2022 kabla ya kucheza mechi ya marudiano nchini Tunisia Novemba 9,2022.

Club Africain itakuwa inarejea nchini Tanzania, kwani katika Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho iliitoa Kipanga ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 7-0.

Katika mechi ya kwanza ilipigwa katika dimba la Aman jijini Zanzibar, Kipanga ilionesha mchezo mzuri ambao uliwawezesha kutoa sare.

Aidha,Yanga SC imefikia hatua hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa pili wa marudiano uliopigwa katika dimba la Al-Hilal jijini Omdurman, Sudan hivi karibuni.

Al Hilal walimaliza hesabu dakika ya tatu kupitia kwa Mohamed Abdel Raman baada ya mabeki wa Yanga SC kufanya makosa na kuifanya timu hiyo kuondolewa kwa jumla ya mabao 2-1.

Ni kufuatia mechi ya kwanza ambayo ilifanyika katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Oktoba 8, 2022 kufungana bao moja kwa moja.

Safari ya Yanga SC ilizimika licha ya kuonekana kucheza vizuri tangu mwanzo wa mchezo ila ilishindwa kuvunja rekodi yake ya kutinga hatua ya makundi kwenye michuano baada ya mwaka 1998.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news