Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameteua viongozi mbalimbali leo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 3, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said.

Mosi, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Khamis Haji Juma kuwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo, Khamis alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Pili,Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Hafidh Ali Mohamed kuwa Afisa Mdhamini wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Pemba. Hafidh Ali Mohamed kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alikuwa Afisa wa Tume ya Uchaguzi.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Gharib Haji Kombo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Kabla ya uteuzi huo, Gharib alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais-Ikulu.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Rashid Hamdu Makame kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Kabla ya uteuzi huo, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Mhandisi Zena A.Said, Rashid alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais-Ikulu.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Nasriya Mohammed Nassor aliyekuwa anashika wadhifa ho atapangiwa kazi nyingine.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Said Khamis Salim kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi wa Said alikuwa Msaidizi wa Rais-Hotuba.

Sita, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Mohamed Juma Abdalla kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. Dkt.Mohamed aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Novemba 3, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news