TANZIA:Mtumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) afariki


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) anasikitika kutangaza kifo cha Ndg. Gerald Mwanilwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, kilichotokea tarehe 02 Novemba, 2022 nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mipango ya Mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Ilazo, jijini Dodoma. Kwa masikitiko makubwa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake
lihimidiwe.

Post a Comment

0 Comments