Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Sahrawi atembelea Mji wa Serikali Mtumba

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Sahrawi, Mhe. Brahim Ghali leo amefanya ziara ndogo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambapo alitembelea jengo la Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu, Bw.Omar S Ilyas pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw.Meshack Bandawe wakimuonesha Mhe. Rais Brahim Ghali maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba.

Katika ziara hiyo ndogo, Mhe. Rais Brahim Ghali alikaribishwa na kuoneshwa Mji wa Serikali na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu,Omar S Ilyas, pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw.Meshack Bandawe, ambapo walipata nafasi ya kuoneshwa kiwanja cha Ubalozi wa Taifa la Watu wa Sahrawi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu, Bw.Omar S Ilyas, pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw.Meshack Bandawe wakimuonesha Mhe. Rais Brahim Ghali maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba.(Picha na OWM).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news