Kuiona Simba SC dhidi ya Al Hilal ni 2000/- leo

NA DIRAMAKINI

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ametangaza viingilio vya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni ambapo cha chini kitakuwa shilingi 2000.
Ahmed amesema, viingilio hivyo vinatokana na awali kucheza mechi ya ligi na watu walilipa hivyo ili kuwapunguzia majukumu tumeweka kiingilio kidogo ambacho kila mtu atakimudu.

Ahmed aliongeza kuwa,leo itakuwa siku ya mtoko wa mwisho wa wiki kwa hiyo Wanasimba wanapaswa kufika uwanjani kufurahi na familia ambapo watoto chini ya umri wa miaka 10 wataingia bure.

Viingilio vilivyopangwa

VIP A Sh. 10,000
VIP B Sh. 5000
Mzunguko 2000

Hayo yanajiri ikiwa juzi, kikosi cha Simba SC kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Jean Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya nane baada ya kumaliza mpira wa adhabu uliopigwa na Chama.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 20 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Chama.

Bruno Gomes aliwapatia Singida bao la kwanza dakika ya 34 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango, Aishi Manula.

Pape Sakho alitupatia bao la tatu dakika ya 63 kwa tik tak baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

Post a Comment

0 Comments