Rais Dkt.Samia afanya uteuzi REA,EWURA,TIC,TTB na Makamishna wa Tume

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 3,2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus.

Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bi. Janet Zebedayo Mbene kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. James Andilile Mwainyekule kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Bw. Mwainyekule ni Mhasibu Mkuu, Tume ya Pamoja ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma.

Amemteua Bw. Rashid Kassim Mchatta kuwa Skauti Mkuu Tanzania. Bw. Mchatta anachukua nafasi ya Bi. Mwantumu Mahiza ambaye muda wa kutumikia nafasi hiyo umemalizika.

Amemteua Bw. Gilead John Teri kuwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Bw. Teri ni Mshauri Mwandamizi, Umoja wa Ulaya (EU), Copenhagen, Denmark.

Amemteua Bw. Damasi Joseph Mfugale kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Bw Mfugale ni Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Afrika Chapter EBI International Consulting Group, Canada.

Amewateua Makamishna wa Tume wawili (2) kama ifuatavyo:-

Bi. Caroline Joseph Mutahanamilwa kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania; na

Bw. Idd Ramadhan Mandi kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,uteuzi huu umeanza tarehe 1 Februari, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news