MKURUGENZI MPYA WA NHC AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA ARDHI

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mkuu mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukioongozwa na Waziri wa wizara hiyo, Dkt.Angeline Mabula.
Viongozi hao wamekutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 13 Machi 2023 katika ofisi za wizara zilizopo katika mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.
Viongozi aliokutana nao Mkurugenzi Mkuu wa NHC ni pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Geofrey Pinda na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga.
Bw. Hamad Abdallah ameteuliwa hivi karibuni kuwa mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa kuchukua nafasi ya Nehemiah Mchechu aliyeteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news