Simba SC yasema Vipers hawatoboi leo

NA DIRAMAKINI

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Ahmed Ally amesema, hakuna jambo jingine wanalihitaji zaidi ya ushindi katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa leo Jumanne katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Ahmed amesema, ushindi dhidi ya Vipers utawaongezea nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali kwa kuwa watakuwa wamefikisha alama sita.

Pia Ahmed amesisitiza kuwa ushindi dhidi ya Vipers ni jukumu la Wanasimba wote kuanzia viongozi, benchi la fundi, wachezaji mpaka mashabiki na kila mmoja anapaswa kutimiza nafasi yake.

“...tuna jukumu zito Wanasimba, tunahitaji kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu. Ni matumaini yetu kila mmoja akitimiza jukumu lake Vipers hatoboi.

“...tumeteua jukwaa la chini ya TV kubwa pale kwa Mkapa, vikundi vyote vya hamasa vitakaa pale au yoyote anayejiweza hatuta pumzika dakika zote 90,” amesema Ahmed.

Post a Comment

0 Comments