Tulieni, tutampiga mtu leo

NA DIRAMAKINI

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema wamepata wiki moja maandalizi ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Robertinho amesema kitu kizuri kinachomfurahisha ni jinsi hali ya kujiamini kwa wachezaji na wanavyojituma mazoezini.

Kocha Robertinho ameongeza kuwa, mpaka sasa tayari anacho kikosi cha wachezaji 11 waliofiti ambao wataanza kwenye mchezo wa leo.

“Mimi ni mtu chanya siku zote, nina muamini Mungu, nawaamini wachezaji wangu, nina miezi mitatu tangu niwe hapa, lakini tumeanza kubadilika kiuchezaji.

“Vipers ni timu nzuri, inacheza soka la kushambulia kwa kushtukiza, tumefanya maandalizi ya kuwadhibiti ili tupate ushindi. Ninaamini hatua kwa hatua tunaweza kuvuka na kuingia robo fainali,” amesema Robertinho.

Kwa niaba ya wachezaji, mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amesema wamejipanga kuhakikisha wanarudisha heshima ya Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kupoteza mchezo uliopita.

“Tumeanza vibaya mashindano haya msimu huu lakini wachezaji tumejiandaa, tunajua tuna jukumu zito, tunaenda kucheza kwa kutafuta pointi tatu lakini tunachukua tahadhari kwakuwa Vipers ni timu bora.

“Hatuna presha sababu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Raja, tumeandaliwa vizuri kimwili na kiakili na tuna imani tutarudisha heshima kwa kushinda, tupo tayari kupambana kwa ajili ya kupata pointi tatu,” amesema Kapombe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news