Tuuishi Ukristo kwa matendo

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa wanapaswa kuyashika mafundisho ya Yesu kwa kuishi ukristo wao kwa mawazo, maneno na matendo na hayo yatawezekana kwa kuyashika mafundisho yake ambapo mojawapo ya mafundisho ya Yesu ni kuzishka amri Kumi za Mungu na upendo.
Hayo yamesemwa na Padri Alex Sivano katika Kanisa la Bikira Maria Malikia wa Wamisionari, Parokia ya Malya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, katika misa ya pili ya Jumapi ya Saba ya Pasaka ikiwa ni Sherehe ya Kupaa kwa Bwana, ndani ya mwaka A wa Liturjia ya Kanisa. 

“Katika jumapili hii ya kupa kwa Bwana tuishi kwa kutenda mema kwa mambo yote na lazima pawepo na utafauti kwa yule anayekuja kanisa kusali na yule asiyefika kanisani. Hapo tutaishi Ukristo wetu kwa wema.” 
Akiendelea kuhubiri katika misa hiyo Padri Alex Sivano ambaye ndiye Mkurugenzi wa Chuo cha Makatekista Bukumbi aliongeza kuwa iwe kwa watoto, iwe kwa vijana , iwe kwa wazazi na iwe kwa mtu yoyote yule anapaswa kuishi kwa matendo mema ambapo alibainisha kuwa hata watoto wadogo katika familia zetu wanafahamu namna nzuri ya kuuishi Ukristo wetu. Aliongeza kuwa hoja siyo kubatizwa tu bali hoja kubwa ni kuizshika Amri Kumi za Mungu. 

Misa hiyo iliambatana na nia na maombi kadhaa na mojawapo wa maombi hayo ni, “Ulitimiza wokovu kwa wote, kwa hiyo umekabidhiwa mamlaka yote Mbinguni na Duniani, utujalie kuonja na kufurahia mamlaka yako katika maisha yetu, ee Bwana twakuomba.” 
Wakati wa matangazo ndani ya misa hiyo Masista watatu wa Shirika la Wabeneditine Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza walipewa nafasi ya kuchangisha michango kwa ajili ya jubilee yao ambapo Sista Mari aShija OSB alisema, 

“Kama shirika tuna Jubilee ya miaka 25 tukiwa Mwanza, Februari 10 1998 Hayati Baba Askofu Antony Mayala alianzisha shirika letu kukiwa na masita watatu tu lakini hadi sasa tupo masista zaidi ya 100. Tupo mbele yeni kama wazazi wetu, kama ndugu zetu na kama wanafamilia ya Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza tunaomba chochote ulichonacho mtusaidie kufanikisha Jubilee hiyo.” 
Mara baada ya maneno hayo michango kadhaa ilichangishwa.Kwa ujumla hali ya hewa ya Malya na viunga vyake kwa juma zima hadi misa hiyo ya pili inakamilika jua limekuwa kali, hakukuwa na mvua, manyunyu wala mawingu huku baadhi ya wakulima wakiendelea na kuvuna mpunga mashambani , nayo mabonde kadhaa yanayolimwa mpunga huo yakiwa na maji ya kutosha. Nayo maji katika mabonde hayo yamekuwa msaada mkubwa kwa maotea ya mpunga kuendelea vizuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news