OR-TAMISEMI yatoa maagizo kwa maafisa elimu nchini

NA JAMES MWANAMYOTO
OR-TAMISEMI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali (OR-TAMISEMI), Mhe.Deogratius Ndejembi (Mb) amewaagiza maafisa elimu wa mikoa na maafisa elimu wa sekondari wa halmashauri nchini kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa miradi ya elimu usiku na mchana ili ikamililike ifakapo Agosti 2023 na kuwawezesha wanafunzi wa kidato cha tano kupata miundombinu bora ya elimu.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI), Mhe. Deo J. Ndejembi (Mb) akizungumza na Maafisa Elimu wa Mikoa na Maafisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri nchini (hawapo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha tathmini ya Utekelezaji wa shughuli za elimu kilichofanyika mkoani Tabora leo Juni 23, 2023.

Mhe.Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo mkoani Tabora wakati akifungua Kikao kazi cha Maafisa Elimu wa Mikoa na Maafisa Elimu wa Halmashauri cha Tathmini ya Utekelezaji wa shughuli za elimu kwa mwaka
2022/23.
Amesema, Serikali kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 7.5 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarasa na Matundu ya vyoo katika Shule za Sekondari za Kidato cha Tano na Sita.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI), Mhe. Deo J. Ndejembi (Mb) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde mara baada ya kufungua Kikao kazi cha Maafisa Elimu wa Mikoa na Maafisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri nchini kilichofanyika Mkoani Tabora, Juni 23, 2023.

“Tumtie nguvu Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo usiku na mchana na kuhakikisha inakamilika ili wanafunzi wa kidato cha tano watakaoripoti shuleni wawe na miundombinu ya kutosha kulingana na idadi yao,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Mhe. Ndejembi amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI haitamfumbia macho yeyote atakashindwa kusimamia na kukamilisha miradi hiyo ifikapo mwezi Agosti 2023, kwani atakuwa ameshindwa kutekeleza wajibu wake
kikamilifu.

Aidha, Ndejembi amesema Serikali kupitia mradi wa SEQUIP imetoa shilingi bilioni 21.18 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika shule mpya 212 za Sekondari za Kata pamoja na Shilingi Bilioni 48 kujenga Shule za Wasichana za Bweni za Mikoa katika mikoa 16.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI),Mhe. Deo J. Ndejembi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wanaosimamia elimu kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Maafisa Elimu wa Mikoa yote mara baada ya ufungua Kikao kazi kilichofanyika Mkoani Tabora, Juni 23, 2023.

Sanjari na hilo, amewataka Maafisa Elimu kufuata taratibu zilizobainishwa katika kusimamia shughuli zote za Elimu ipasavyo ikiwemo ujenzi wa shule mpya na miundombinu inayojengwa katika maeneo yao.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde akimkaribisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI), Mhe. Deo J. Ndejembi kufungua Kikao kazi cha Maafisa Elimu wa Mikoa na Maafisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri nchini kilichofanyika Mkoani Tabora, Juni 23, 2023.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt.Charles Msonde amesema katika Kikao kazi hicho watajadili kwa kina kuhusu namna bora ya usimamimizi na utekelezaji wa miradi elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ikamilike na kuleta tija kwa wananchi na maendeleo ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news