Rais Dkt.Samia afanya uteuzi OR-TAMISEMI, Maliasili na Utalii,TANROADS

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewateua wafuatao:-
i) Amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

ii) Amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Mhandisi Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (CASSOA).

Mhandisi Besta anachukua nafasi ya Mhandisi Rogatus Hussein Mativila 
ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.

iii) Amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii. 

Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Bw. Anderson Mutatembwa ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); na

iv) Amemteua Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus leo Juni 13,2023 uteuzi huu umeanza Juni 12, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news