Singida Fountain Gate, Simba SC mguu sawa Ngao ya Jamii

DAR ES SALAAM-Kikosi cha Simba SC kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Alhamisi katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Kwa mujibu wa klabu hiyo, wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa Alhamisi.

Baada ya mazoezi hayo kikosi kinajiandaa na safari ya Tanga kamili kwenda kushiriki michuano ya Ngao ya Jamii ambayo safari hii inashirikisha timu nne. Mbali na Simba na Singida Fountain Gate wengine ni Yanga SC na Azam FC zote za jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news