Benki ya Dunia yaguswa na ufanisi wa Mahakama ya Tanzania

NA INNOCENT KANSHA
MAHAKAMA

MTENDAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel ameuhakikishia Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuwa Mahakama ya Tanzania itaendelea kutekeleza shughuli za mradi huo kwa kasi iliyokusudiwa na kwa ufanisi mkubwa ili kufanikisha adhima ya kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya utoaji haki nchini.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimuonesha Bango la miradi ya Maboresho inayotekelezwa na Mahakama nchini Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon (kulia) walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Dar es salaam. 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akifafanua mambo mbalimbali yanayohusu shughuli zinazofanyika za maboresho ya Mahakama ya Tanzania wakati alipotembelewa na Ujumbe wa Banki ya Dunia Ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam leo tarehe 07 Septemba, 2023.

Akizungumza na ujumbe huo uliomtembelea Ofisini kwake ukiongozwa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Septemba, 2023, Prof. Ole Gabriel amesema katika kuhakikisha Mahakama inajenga mfumo imara wa utoaji haki nchini ni lazima ishirikiane kwa karibu na wadau wote wanaoshirikiana nao katika shughuli za utoaji haki ili kuimarisha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyenyoosha mkono) akielezea jambo wakati alipotembelewa na Ujumbe huo Ofisini kwake, kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon.

“Hivi karibuni Mahakama ya Tanzania imengia makubaliano hayo na wadau wake ili kuimarisha mfumo wa utoaji haki na kusaidia mifumo kusomana, taasisi hizo ni pamoja na Ofisi ya Mashitaka ya Taifa, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Wakala wa Ufilisi, Vizazi na Vifo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na Wiziara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hii itasaidia kuwarahishia Majaji na Mahakimu kutekeleza wajibu wao,"amesema Mtendaji Mkuu. 
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon (kushoto) na Mtaalum Kiongozi wa Utawala kutoka Banki ya Dunia, Bi. Donna Andrew wakifuatilia mazungumzo hayo walipokuwa wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) Ofisini kwake.

Prof. Ole Gabriel amesema muunganiko huo wa kitehama utachangia kuleta mageuzi makubwa katika tasnia ya utoaji haki nchini. Lakini mafanikio yote hayo muhimu niliyoyataja kwa Mahakama ya Tanzania yasigeweza kufikiwa kirahisi bila jitihada za Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania kuiwezesha Mahakama kupiga hatua hiyo kubwa. 

“Ukiongelea Mradi wa Benki ya Dunia kwetu Mahakama unatazama maboresho mbalimbali sio tu Fedha, Majengo, magari na uondoshaji wa mashauri mahakamani, bali ni matokeo ya kitehama yakieleweka vema kwa jamii yatasaidia kubadili mtazamo wa watu wakiwemo wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuona ni jinsi gani Mahakama inavyowajibika kwa uwazi katika shughuli zake,”alifafanua Mtendaji Mkuu. 
Mtaalum Kiongozi wa Utawala kutoka Banki ya Dunia kutoka Tanzania, Bw. Benjamin Mtesigwa (kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo, kushoto ni Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt akifuatilia.

Prof. Ole Gabriel akauambia ujumbe huo kuwa, katika kuhakikisha Mahakama inajipima imekuwa ikiitumia Taasisi binafsi ijulikanayo kama REPOA kwa ajili ya kufanya utafiti ili kujua kiwango cha kuridhika kwa wateja wa ndani na wa nje ili kupima maboresho yanayoendelea kutekelezwa. 

Utafiti huo ulifanyika katika awamu tatu kwa vipindi vya miaka minne minne kuanzia mwaka 2015 kiwango cha kuridhika kwa wateja kutokana na huduma za Mahakama ilikuwa asilimia 61 ikilinganishwa na mwaka 2019 kiwango kilipanda kwa asilimia 78 na mwaka 2023 kiwango cha kuridhika kwa mteja kimepanda maradufu kwa kufikia asilimia 88, tafsiri yake ni kuwa Mahakama inatoa huduma za uhakika kwa wateja na wadau wake kwa kiwango kikubwa. 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel aliyeshika matoi ya kuchezea watoto akielezea namna yanavyosaidia kuratibu shughuli za watoto wanaofikishwa Ofisini hapo, kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon akimsikiliza.

Kwa upande mwingine, Prof. Ole Gabriel akaelezea mafanikio yanayotokana na uanzishwaji wa Mifumo ya Mrejesho wa Huduma kwa Mteja ya kielektronik na kituo cha huduma kwa mteja kwa njia ya kupiga simu, iliyoisaidia Mahakama kuendelea kupima utendaji wa utoaji huduma kwa kuangalia namna bora ya kuimarisha utoaji huduma ya haki kwa wananchi. 

Mifumo hii imechangia kwa kiasi kikubwa kujua wateja wanakwama wapi na kutatua changamoto kwa haraka, ikiwa ni matokeo ya uboreshaji wa huduma. 
Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu na Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Angelo Rumisha akisoma ripoti ya utekelezaji wa Miradi ya maboresho ya Mahakama nchi inayowezeshwa na Banki hiyo wakati Mahakama ilipotembelewa na Ujumbe wa Banki ya Dunia, kushoto wanafuatilia ni sehemu ya Viongozi wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa maboresho, Naibu Masajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mary Moyo na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mhe. John Chacha.

Mtendaji Mkuu akaumbia ujumbe huo kuwa, kupitia mradi wa maboresho wa Banki ya Dunia, Mahakama imefanikiwa kuanzisha huduma ya Mahakama Inayotembea, kwa sasa huduma hiyo inatolewa katika majiji mawili ya Mwanza na Dar es Salaam na kufanikiwa kuwafikia wanufaika wapatao takribani elfu 45 hadi sasa toka kuanzishwa kwake mwaka 2019, na katika mpango wa awamu ya pili wa maboresho Mahakama imepanga kununua mahakama zinazotembea sita ili kuendelea kuwafikia watu wengi zaidi na kutanua wigo wa kutoa haki katika maeneo mengine yenye uhitaji. 
Sehemu ya Viongozi waandamizi kutoka Mahakama ya Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango na wengine kutoka ujumbe wa Banki ya Dunia wakiongozwa na Jajiv Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (wa kwanza kushoto mstari wa nyuma) wakifuatilia majadiliano ya ripoti hiyo. 

“Maboresho pia yamesaidia kuondosha mlundikano wa mashauri mahakamani kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kuunda vikosi kazi vya Majaji na Mahakimu kupambana na mlundikanao takwimu zinaonyesha mwaka 2015 mrundikano wa mashauri mahakamani ulikuwa asilimia 13 ya mashauri yote yaliyosajiliwa, lakini kufikia mwaka 2023 mwezi Juni mlundikano umefikia asilimia tatu (3), hii yote ni kutokana na msaada mkubwa tunaowezeshwa na mradi wa Banki ya Dunia wa kujengea watu wetu uwezo wa kutumia rasilimali tulizonazo,"aliongeza Prof. Ole Gabriel. 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo yanayotokana na utekelezaji wa miradi ya maboresho ya Mahakama nchini kwa kushirikiana na Banki ya Dunia mara baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya utekelezaji huo, kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon na kushoto ni Mtaalum Kiongozi wa Utawala kutoka Banki ya Dunia, Bi. Donna Andrew wakimsikiliza.

Mtendaji Mkuu huyo, akazungumzia matarajio ya Mahakama katika kuendelea kuboresha huduma za hutoaji haki kwa kufafanua mambo kadhaa ikiwemo; matumiazi ya mfumo wa Akili Bandia utakao rahisisha uendeshaji wa mashauri, kupanua wigo wa mfumo wa TEHAMA ili uweze kutumika katika Mahakama za Mwanzo nchini, kwani takwimu zinaonyesha asilimia 70 ya mashauri yapo katika Mahakama hizo. 
Mratibu wa Mahakama Inayotembea na Mkurugenzi Msaidizi wa Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania, Mhe. Moses Ndelwa akielezea taratibu mbalimbali za uendeshaji wa Mahakama hizo alipotembelewa na Ujumbe kutoka Banki ya Dunia katika ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon (aliyenyoosha mkono) akiuliza swali lilitokana na uwasilishaji wa ripoti ya utekelezaji wa shughuli zinazotokana na miradi ya maboresho ya Banki ya Dunia. 

Pia kuboresha zaidi mfumo wa kusimamia mashauri “Advance Case Management” ili kuongeza ufanisi na umakini katika kufanya mambo kwa usahihi na kutunza takwimu za mashauri, kuongeza miundombinu ya kisasa ya kufanyia kazi hii itaongeza kujiamini kwa watumishi wanapotekeleza majukumu yao na kuongeza ubunifu wa kufikiri na kuboresha usawa wa kijinsia na mambo mengine. 
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon akielezea kufurahishwa kwake na jitihada kubwa zilizofikiwa na Mahakama ya Tanzania katika kuboresha mfumo wa haki nchini kupitia uwezeshaji wa mradi wa Banki ya Dunia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon akaushuru Uongozi wa Mahakama kwa kuendelea kushirikiana na Banki ya Duania katika safari ya kutekeleza mambo makubwa yenye mafanikio kwa wananchi yanayolenga kuboresha mifumo ya utoaji haki nchini kupitia mradi wa Banki ya Dunia. Ni jambo la kuvutia kuona mambo yote hayo yaliyotajwa yametokana na jitihada za mradi huo ni jambo la kuvutia. 
Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Happiness Nyange (kulia) anayetoa huduma ndani ya Mahakama Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia, akielezea namna anavyotoa huduma kwa watoto wenye uhitaji alipotembelewa na Ujumbe kutoka Banki ya Dunia.

“Kwa mtazamo wangu mimi mwenye uelewa ndogo kuhusu shughuli nyingi za mifumo ya kimahakama katika sehemu nyingi za dunia hasa kwa nchi zenye kipato sawa na Tanzania ambapo watu wanadanganywa ama kudhurumiwa na mifumo ya kimahakama na huo ndiyo ukweli katika nchi nyingi.” 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon (wa tatu kushoto), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wengine kutoka Banki ya Dunia, uliofika kutembelea Mahakama Inayotembea kujionea shughuli zinazofanywa na Mahakama hiyo Temeke jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Hassan akaipongeza Mahakama kwa kuanzisha mifumo imara ya kusaidia kutoa huduma ya haki kwa uwazi kama mfumo wa huduma ya mrejesho kwa mteja na kuboresha mfumo wa kusimamia mashauri na hivyo kuleta mageuzi na kuonesha utofauti mkubwa sana katika mfumo wa utoaji haki nadhani hayo ni maendeleo makubwa. 

“Ninapotazama kwa ujumla Tanzania ipo katika safari ya ukuaji wa uchumi ukalinganisha na nchi zingine, nafasi ya Mahakama katika kuboresha mifumo yake kama mfumo wa kusimamia mashauri na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na kupunguza hatua za usikilizaji wa mashauri kwa uboreshaji huo utasaidia kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi, mifumo kama hiyo itasaidia kuwalinda wawekezaji katika sekta mbalimbali ndani ya nchi,"aliongeza Mkurugenzi huyo.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akisalimia na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon (kulia) walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Dar es salaam. 

Mkurugenzi Hassan amesema kwa sasa maboresho ya mifumo hiyo ya utoaji haki itaonekana inawasaidia wananchi pekee la hasha bali inaongeza uamininifu si kwa wananchi pekee inakuza jedwali la nchi na kuvutia wawekezaji wa nje wakiamini Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza. Kwa jinsi mifumo ya kimahakama itavyoendelea kuboreshwa ni njia sahihi ya kuendelea kuonyesha ni sehemu salama kwa wawekezaji wengi zaidi na sit u kwa wawekezaji wa nje hata wandani watatamani kuwekeza zaidi. 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka Banki ya Dunia, uliofika Ofisini kwake kufanya mazungumzo, wengine ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Kanda, Bw. Hassan Zamon (wa tatu kushoto), Mtaalum Kiongozi wa Utawala kutoka Banki ya Dunia, Bi. Donna Andrew (wa pili kulia), Mtaalum Kiongozi wa Utawala kutoka Banki ya Dunia kutoka Tanzania, Bw. Benjamin Mtesigwa (wa kwanza kulia), Msaidizi wa Programu kutoka Banki ya Dunia, Bi. Catherine Mutagwa (wa pili kushoto) na Msaidizi wa Programu kutoka Banki ya Dunia, Bi. MaryIrene Singili (wa kwanza kushoto).

“Utawala wa sheria ni kipengele cha msingi katika kukua kwa uchumi wa Taifa lolote na kuleta maendeleo ya kweli na penda nichukue nafasi hii kuipongeza Mahakama kwa maboresho makubwa na ahidi kuendelea kushirikiana nanyi na kutia nguvu katika maeneo yote unayoendelea kufanya maboresho ya kweli,”alisisitiza Mkurugenzi Hassan

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news