Rais Dkt.Mwinyi ateua wakuu wa mikoa, wilaya

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said na uteuzi wao unaanza Novemba 16, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Mheshimiwa Ayoub Mohamed kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Kabla ya uteuzi huo, Mheshimiwa Ayoub alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Rashid Hamid Rashid kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja. Kabla ya uteuzi huo Mheshimiwa Rashid alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Sadifa Juma Khamis kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja. Kabla ya uteuzi huo, Mheshimiwa sadifa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Othman Ali Maulid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja. Ndugu Othman ni mstaafu wa utumishi wa umma.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Galos Nyimbo kuwa Mkuu wa Wilaya Kusini Unguja. Ndugu Galosi ni mwanajeshi mstaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news