Mhandisi Mahundi apelekwa Wizara ya Habari, Katimba ateuliwa OR-TAMISEMI,Sillo ateuliwa Mambo ya Ndani

ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhamisha Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Pia,Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Zainab Athuman Katimba kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mheshimiwa Katimba anachukua nafasi ya Deogratius John Ndejembi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Vile vile,Rais Dkt.Samia amemteua Daniel Baran Sillo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mheshimiwa Sillo anachukua nafasi ya Jumanne Abdallah Sagini ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news