Dkt.Kikwete awasilisha Ujumbe Maalum wa Rais Samia kwa Rais wa Jamhuri ya Congo Brazzaville

BRAZAVILLE-Rais wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo Brazzaville), Mhe.Collinet Makosso Anatole.
Mhe. Anatole alipokea ujumbe huo wa maandishi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Congo , Mhe. Denis Sassou Nguesso ambaye alikuwa kijijini kwao kushiriki mazishi ya kaka yake.

Tukio hilo lilifanyika jijini Brazzaville Aprili 14, 2025 na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili.
Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news