Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA),Mhe. Salum Mwalimu. Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Devotha Mathew Minja (kushoto) alichukua fomu hizo Agosti 12, 2025 ambapo Tume inatarajia kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Kualia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhan Kailima. (Picha na INEC).
Waandishi wa Habari, Salum Mwalimu aliyepata kufanya kazi katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Devotha Minja aliyekuwa mwandishi wa ITV mkoa wa Morogoro wamechukua mkoba wa fomu za uteuzi wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kupitia Chama cha CHAUMA. Wagombea hao pichani wakiwa na mkoba wao wa fomu za uteuzi.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) Mhe. Salum Mwalimu akielekeza namna ya kujaza kitabu.
Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma),Mhe. Salum Mwalimu akisaini kitabu.
Mgombea Mwenza Mhe. Devotha Minja akisaini kitabu.
Mgombea Mwenza Mhe. Devotha Minja akisaini kitabu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kilima akizungumza.
Mwenyekiti wa Chaumma,Mhe. Hashim Rungwe akiwa Benson Kigaila.
Tags
Chama cha CHAUMMA
Habari
INEC Tanzania
Picha
Picha Chaguo la Mhariri
Ratiba ya Kuchukua Fomu INEC