Kuelekea mwaka mpya 2026,REA yawashika mkono wahitaji

DODOMA-Kuelekea Mwaka Mpya 2026, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imewagusa Watanzania wenye mahitaji mbalimbali kwa kutoa mkono wa faraja na kuwatakia heri ya mwaka Mpya ujao.
Zoezi la kuwapatia mahitaji watu wenye mahitaji maalum limeongozwa na Bi. Judith Abdalah kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA,Mhandisi Hassan Saidy ambapo REA imetoa mahitaji mbalimbali kwa Kikundi cha Walemavu wa Ukoma waliopo Kata ya Hombolo jijini Dodoma.

Akiwasilisha salamu za REA, Bi. Abdalah amewataka walemavu wa ukoma kuishi kwa upendo na amani na kusisitiza kuwa, REA itaendelea kuwashika mkono kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ili wakue kiuchumi na kijamii.
Halikadhalika, Swalehe Kibwana Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la REA (TUGHE), amesema zoezi hilo la kuwafikia na kuwasaidia wahitaji mbalimbali ni endelevu na REA itaendelea kutoa mahitaji kwao hususan kwa walemavu wa ukoma waliopo Hombolo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Samia mkoa wa Dodoma,Bi. Fatuma Madudu ameishukuru REA kwa kufika Hombolo na kuwasaidia walemavu wa ukoma katika sehemu hiyo kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali.
Naye, Katibu wa Walemavu Hombolo ametoa rai kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwashika mkono Walemavu wa ukoma na kuwapatia mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula ili nao waweze kufurahia sikukuu ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news