Taifa Stars yafuzu hatua ya mtoano michuano ya AFCON

NA DIRAMAKINI

TIMU ya taifa ya Tanzania ya Taifa Stars imefuzu hatua ya mtoano ya michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza kwenye historia tangu michuano hiyo ianzishwe mwaka 1957.
Stars imefuzu hatua hiyo kwa njia ya "Best Loser" baada ya kumzidi Angola kwenye kigezo cha idadi ya mabao ya kufunga.

Taifa Stars katika hatua ya 16 bora watakipiga dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo Timu ya Taifa ya Morocco.

Katika kundi C Nigeria wamemaliza wakiwa na alama tisa, Tunisia wakiwa na alama sita, huku Uganda wakiwa na alama moja.

Aidha,katika mchezo wa leo Desemba30,2025 uliopigwa ndani ya Prince Moulay Abdellah Stadium uliopo mjini Rabat nchini Morocco, Tunisia walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 42 kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Ismaël Gharbi.

Tanzania walipata bao la kusawazisha dakika ya 48 kupitia Feisal Salum Abdallah (Fei Toto) aliyefunga kwa shuti kali nje ya eneo la mita 18 na kumshinda kipa wa Tunisia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news