ARUSHA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi inayolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma pamoja na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI.
Kabla ya kuanza ziara hiyo ya siku mbili, Prof. Shemdoe mapema leo amefanya kikao kazi na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makala.






