Waziri Mkuu aanza ziara ya kikazi mkoani Songwe

SONGWE-Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba leo Desemba 17, 2025 akizungumza na wakazi wa eneo la Tunduma mkoani Songwe ambapo yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua uharibifu wa miundombinu ya umma na mali binafsi zilizoharibiwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025.
Akizungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaagiza Watendaji Wakuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na TARURA kufanya tathimini ya miradi yote ambayo malipo ya awali yameshafanyika na hatua za ujenzi zilizofikiwa katika miradi hiyo.
Pia, amewaagiza kuangalia kama utekelezaji wa miradi hiyo unaendana na kiwango cha fedha ambacho kimeshatolewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news