Riba ya Benki Kuu yabaki asilimia 5.75 robo ya kwanza 2026


KAMATI ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeamua Riba ya Benki Kuu (CBR) kubaki asilimia 5.75 katika robo ya kwanza ya mwaka 2026 kutokana na matarajio chanya ya ukuaji wa uchumi na mwenendo thabiti wa mfumuko wa bei nchini.
Katika kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) kilichofanyika tarehe 7 Januari 2026, kiliamua Riba ya Benki Kuu (CBR) ibaki kuwa asilimia 5.75 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2026.

Uamuzi huu umefikiwa kwa kuzingatia matarajio ya mfumuko wa bei kuendelea kuwa ndani ya lengo la asilimia 3 hadi 5. 

Hayo yamebainishwa leo Januari 8,2025 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Gavana wa BoT, Bw.Emmanuel Tutuba wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam.

Gavana Tutuba amesema, kiwango hicho cha CBR ni sawa na kile kilichotumika katika robo ya mwaka ulioishia Desemba,2025.

"Uamuzi huo wa kubakiza CBR kama ilivyokuwa katika robo ya nne ya mwaka 2025 utasaidia kuendelea kuchagiza ukuaji wa shughuli za kiuchumi nchini na kuwezesha ukuaji wa uchumi kuwa wa kuridhisha. 

"Kwa kuzingatia uamuzi huu, Benki Kuu itatekeleza sera ya fedha kwa kuhakikisha riba ya mikopo ya siku 7 baina ya benki (7‑day interbank rate) inabaki ndani ya wigo wa asilimia 3.75 hadi 7.75."

Kiwango cha Riba cha Benki Kuu (CBR) ni kiwango kinachowekwa na BoT kama rejea katika utekelezaji wa shughuli zake mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukopesha benki za biashara. 

Kiwango hiki huathiri riba za mikopo baina ya benki za biashara, ambazo zinapaswa kuwa ndani ya wigo wa asilimia 3.75 hadi 7.75 ya CBR iliyowekwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here