Mheshimiwa Ridhiwani akemea tabia za baadhi ya waajiri kuwahamisha watumishi

NA VERONICA MWAFISI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekea tabia ya baadhi ya Waajiri kuwahamisha watumishi wanaowakuta katika Ofisi walizoteuliwa na kutaka wahamishiwe katika vituo vingine vya kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) akisikiliza maelezo kuhusu mifumo mbalimbali wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kabla ya kufunga mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba.

Waziri Kikwete ameyasema hayo leo Februari 19,2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha wakati akifunga rasmi mkutano wa sita wa Serikali Mtandao ulioanza Februari 17, 2026.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza na Maafisa Masuuli, Maafisa TEHAMA na watumiaji wa Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakati akifunga mkutano wa sita wa Serikali Mtandao katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.

Amesema, kama ikitokea mtumishi ana tatizo lolote la kiutumishi linalohitaji hatua za kinidhamu, apelekwe kwenye vikao vya kinidhamu ili adhabu stahiki itolewe na sio kuwaonea watu kwa sababu ya unyonge wao.

"Nataka niwakumbushe kuwa, kila mmoja aliingia kwa sifa zake, wengine wameingizwa kupitia mitihani ya ajira, wengine kwa nafasi za uteuzi, hivyo kila mmoja akitimiza wajibu wake ni wazi kuwa matokeo mazuri yataonekana."
Sehemu ya Maafisa Masuuli, Maafisa TEHAMA na watumiaji wa Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakiwa kwenye mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Aidha, amepiga marufuku watumishi wa umma kutumia barua pepe binafsi kutuma taarifa za ofisi badala ya kutumia barua pepe rasmi za serikali.

"Ni changamoto kubwa sana, bado tunao watumishi wa umma wanaotumia mitandao binafsi kutuma taarifa rasmi za serikali, tunachokifanya ni jambo la hatari sana, tutumie mifumo yetu iliyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani,"Mhe. Kikwete ameongeza.

Waziri Kikwete amewapongeza e-GA kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwasisitiza Waajiri kutumia wataalam hao kutengeneza mifumo katika taasisi zao.

Ametoa wito kwa wataalamu wa TEHAMA kuendelea kujifunza kila wakati ili waweze kukabiliana na changamoto mbambali ikiwemo shambulio la mifumo ya TEHAMA.
Sehemu ya Washirkiki na Wanakamati wa mkutano wa sita wa Serikali Mtandao wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati akitembelea mabanda mbalimbali kabla ya kufunga mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict Ndomba.
Akitoa salamu kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Waziri Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuishirikisha kamati hiyo.

"Mmetambua uwepo wa mhimili wa Bunge, mngeweza hata kufanya wenyewe bila hata ya kutushirikisha," ameongeza Mhe. Dkt. Ndumbaro.

Amesema, yeye sio mtaalam wa TEHAMA, lakini bado anatambua umuhimu wa serikali mtandao na kuongeza kuwa, kwa dunia ya leo hatuwezi kusonga mbele bila ya TEHAMA.

Amesema, Tanzania imepata mafanikio makubwa ambayo yanatokana na kazi nzuri ya Serikali kupitia Chama Cha Mapinduzi pamoja, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

“Sisi kama kamati na Bunge tunatambua mafanikio hayo. Mafanikio ya kupeleka huduma kwa umma, kunganisha mifumo, kutuhakikishia usalama mtandaoni ni kazi nzuri yenye mafanikio makubwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati akielekea kutembelea mabanda mbalimbali kabla ya kufunga mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya AICC Arusha kwa ajili ya kufunga mkutano wa sita wa Serikali Mtandao.

"Tuko tayari kushirikiana na Wizara kuhakikisha changamoto zinazohusu sera, sharia na bajeti zinafanyiwa kazi. Kila mawasiliano ya Bunge yanakwenda kwa mtandao."

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Mhandisi Benedict Ndomba amemshukuru Waziri Kikwete pamoja na uongozi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa maelekezo na msisitizo kuhusu uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwani vimeongeza uzito, mwelekeo na ari mpya kwa washiriki wote.

"Tunathamini sana mchango wako na w viongozi wote katika kuendeleza ajenda ya mageuzi ya kidijitali Serikalini,"Mhandisi Ndomba amesisitiza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here